Nyimbo Mpya: Best Naso Aachia Video Mpya ‘Mwambie’

[Picha: Best Naso Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa Bongo Best Naso ameachia kanda ya wimbo wake mpya kwa jina “Mwambie”. Huu ni wimbo wa mapenzi ambao unaelezea machungu alopitia mwanuame mmoja kwa sababu ya kupenda.

Katika hadithi hii ya “Mwambie” Best Naso anataka mpenzi wake aambiwe kuwa hana raha tangu binti anayempenda alivyomuacha.

Soma Pia: Nyimbo Tano za Mduara Zilizovuma Bongo

Katika mistari yake Best Naso anataka rafiki zake waende wamuongeleshe Shamela ajue kua anampenda sana. Naso anatishia kujiua iwapo Shamela hatampenda yeye kwa kusema ni yeye tu anamfaa.

“Maringo na kiburi kanifanya naimba, mwambie sina raha,ana pozi masahuzi yeye ndio ananifaa (Shamela) Kiukweli nampenda, Nikimkosa mi nitachizi…” aliimba Naso.

Hata hivyo kanda hii inaonyesha kuwa Shamela hampendi Naso kwa sababu hawezi mtosheleza kihela.

Kanda hii imetayarishwa kwa ujuzi mkubwa na mwelekezaji kwa jina Mato huku mdundo wa wimbo ukifanywa na King Fenya na Duper. Best Naso ni mojawapo ya wasanii tajika wa Bongo ambao kwa sasa hawajapata fursa kubwa sana ya kuonyesha talanta zao.

Soma Pia: Zuchu Aweka Rekodi Mpya YouTube Tanzania

Best Naso anajulikana kwa wimbo wake "Nirudi Kijijini" uliompa sifa miaka michache iliyopita.

Hivyo kimbilio lake kwa sasa ni kuachia tu ngoma mpya akitumaini kuafikia malengo tena. Kufikia sasa wimbo huu “Mwambie” unaendelea kupokelewa vizuri kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=eiiYRlsyk4Q

Leave your comment