Nyimbo Tano za Mduara Zilizovuma Bongo
27 March 2021
[Image Source: Instagram - Offsidetricktz]
Get Free Music Updates and Mixes on Telegram
Mduara ni moja wapo ya fani za mziki kutoka Tanzania zilizovuma kwa sana miaka michache iliyopita. Tunapoendelea kusiifia nyimbo za Tanzania, katika nakala tunaangazia nyimbo tano bora za mduara zilizovuma bongo.
Lawama Ya Shilole ft Q Chila
Hii ni kazi yake Shilole akimshirikisha Q Chilla. Huu ni wimbo uliongazia maneno watu wanaopenda kutupa lawama kwa watu wengine. Kwa wimbo ulioachiwa miaka kadhaa iliyopita, ni wimbo ulio na maudhui tunayoweza kuendana nayo hata leo. Kufikia sasa kwenye mtandao wa YouTube ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya Laki Tisa.
Bi Harusi Yake AT
Kutoka Kwetu Studios, At aliachia kazi hii kuwaonya wanawali wanaopenda kujionyesha tu bila ya kujisitiri. Aanendelea kuwaonya waschana wanoelewa dhidi ya kukashifu wakwe zao. Yote tisa ni wimbo wa mafunzo ya ndoa.
Vifuu Tundu ya AT FT Mwa4
Huu ni wimbo wa michambo amapo AT anawaonya wambea wanaosema yasowahusu. Vifuu tundu wanapenda kusema yasio na maana yoyote. Ngoma hii ya mduara ni utungo mahususi kutoka kwa albamu yake AT iitwayo “Asili Haipotei”.
Nasema Nawe ya Daimond Platnumz ft Khadija Kopa
Hii ni kazi yake Diamond Platnumz aliyomshirikisha Khadija kopa katika kuwaonya watu wanaopenda kuchepuka. Kazi hii ilimpa Diamond Uaarafu zaidi haswa katika kuwa na ujuzi wa kufanya aina zote za mziki hii ikiwa mduara. Kufikia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya milioni thelathini na moja.
Kidudu mtu ya Offside Trick ft Mwa 4
Huu ni wimbo pia unaongazia wambea ambaye nia yake ni kuwakosanisha wattu katika jamii. Offside Trick walipata fursa kuwaonya watu dhidi ya kuwa na roho mbaya .
Leave your comment