Harmonize Aelezea Hofu ya Kifo cha Magufuli na Uoga Alionao

youtube

Mwandishi: Branice Nafula

Join Us on Telegram

 Mkurugenzi mkuu wa Konde Music Worldwide Harmonize ni mmojawapo wa watu ambao wameathiriwa sana na kifo cha Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ambaye alifariki kwa shida ya moyo.

Harmonize amefunguka juu ya hofu yake ya kifo. Harmonize Kupitia mtandao wa Instagram, alisema haya baada ya kwenda kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu kwenye Uwanja wa Uhuru.
“Usiku Nilipata Taarifa Ya Kifo Chako ...!!! Moyo wangu Ulisita Kukubaliana na hali Hiyo Lakini Akili iliamini…Uchungu na Masikitiko Makubwa Yalinipeleka Mbali na Kuwaza Mengi Mno Mpaka Kufikia Kiasi nikasema Kama Nilikuwa Nikikuimbia Ukiwa Hai Na Kufurahia Sauti na Tungo Zangu Nyingi Zakukupongeza Basi Sina Budi Kukuimbia Ikawa Umelala na Hauwezi Amka Tena...!!!!” aliandika Harmonize

Awali Harmonize alikashifiwa kwa kurekodi video huku akilia baada ya kupata habari ya kifo cha rais huyo.

Akiwa miongoni mwa wasanii walioenziwa na Hayati Magufuli amabayo kwa Kiasi alikua pia miongoni mwa wasanii waliomsaidia rais huyo katika kampeni za kura hapo mwaka jana.
Harmonize alielzea kuwa kumuona Hayati kwenye jeneza ilimpa uoga zaidi hata kama alijua kila binadamu njia yae ya mwisho ni kifo.

“Isipokuwa Mungu wa Mbinguni Kwa Hali Ya Masikitiko Sanaa Mimi Kijanawako na Vijana Wenzangu Tukajikusanya Kwa Majonzi na Kutengeneza wimbo Huu Tunaamini Maumivu na Majonzi Tulionayo Wenda Yanaweza Kuzaa Sauti Ya Kukuombea Msamaha Mbele Za Mungu na kukupumzisha Mahala Pema (PEPONI ) hata hivyo Bado Moyo Haukutaka Kuamini Mpaka Nilipokuona Umelala Kwenye JENEZA Jana UWANJA WA UHURU Naamini Kila Mwanadamu Atakufa Ila tulio wengi tunakiogopa Kifo Mpaka Kupelekea Kuogopa Mtu Alie Kufa Mimi Ni Miongoni Mwao NAOGOPA na naona ni Tendo La Ajabu Na Silipatii Tafsiri ingawa ni Tendo La LAZIMA ila Jana Nilikuja Kukuona Ili Nijirizishe Kama ni Kweli...” alimalizia Harmonize.

Harmonize na wasanii wake katika Konde Music waliachia wimbo wa kumuomboleza rais huyo kwa jina “Asante Magufuli”.

Download Harmonize Music FREE

https://www.youtube.com/watch?v=CqEvlLonyB8

Leave your comment