Nyimbo Mpya: Anjella Aaachia ‘Kama’ Akimshirikisha Harmonize

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msani mpya wa lebo ya Konde Music Worldwide Anjella hatimaye ameachia rasmi wimbo wake wa kwanza kwa jina "Kama", akimshirikisha Harmonize.

“Kama” ni kazi yake ya kwanza ndani ya lebo hiyo. Wimbo huu ni wa maudhui ya mapenzi ambapo waimbaji hao wanaangazia hulka na tabia za watu wanaotaka kuwa na uhusiano nao.

Soma Pia: Diamond Platnumz: Nilijifunza Muziki Kupitia Nyimbo Zake Barnaba Classic

Anjella anaanza kwa kumuomba Mungu ampe mtu mwenye mapenzi ya kweli na si wa kumuhadaa.

Anelezea uchungu atakaohisi iwapo mpenzi wake atamdanganya. “Ahahaha Jeshi Sounds by Abbah (Konde Boy) Kwanza namuomba Mungu iwe kweli Nipate wa kunipenda anirithie kwa moyo niepushe na matapeli,wale wa kula na kwenda mi nmeumbwa na choyo…” hii ni baadhi ya mistari kwenye wimbo huu.

Pakua Nyimbo Zake Harmonize Bure Kwenye Mdundo

Vile vile anaazimia kupendwa hadi atakapopelekwa nyumbani kwa wazazi. Harmonize naye anaingia kwa kusema kuwa uzuri wa mke ni tabia, huku sura na shepu ni vya kuchangia tu.

Kwa mwanamziki anayejaribu kuingia katika fani iliyojaa tayari, Anjella anastahili kupewa heko kwa motisha aliyonayo.

Soma Pia: Pakua Mixtape 5 Mpya za Muziki Bora Machi 2021

Kwa sasa, wimbo huu unaendelea kufanya vizuri kwenye mitandao ya kuskiliza mziku huku kwenye YouTube ikipata watazamaji zaidi ya laki moja.

Kanda ya wimbo huu inatarajiwa hivi karibuni huku mwandalizi wa wimbo huu akiwa Abbah Process.

https://www.youtube.com/watch?v=z2LHODzQ1JA&ab_channel=Anjella

Leave your comment