Nyimbo 5 Bora za Lava Lava Tangu Ajiunge na WCB [Video]

[Picha: Biggest Kaka]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Kwenye WhatsApp

Msanii Lava lava ni moja wapo wa wasanii tajika kutoka lebo ya WCB. Anajulikana kwa kufanya kazi nzuri hasa kwenye nyimbo za mapenzi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Weusi Wamshirikisha Khadija Kopa Kwa Wimbo Wao Mpya ‘Penzi la Bando’

Uandishi na ushairi wake umewapendeza wengi na kuwafanya wawe mashabiki zake. Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo tano bora zaidi za Lava lava tangia ajiunge na lebo ya Wasafi:

Tuachane

Huu ulikua wimbo wake wa kwanza uliomtambulisha Lava lava katika lebo ya Wasafi mwaka 2017. ‘Tuachane’ ni wimbo wa mwanamume aliyeumizwa katika mahusiano yake na mrembo aliyekuwa amempenda sana. Kufikia sasa ni wimbo wake mkubwa zaidi na una watazamaji zaidi ya milioni kumi na tatu.

https://www.youtube.com/watch?v=BJ9FLAnEUg4

Gundu

‘Gundu’ ni wimbo unaoangazia uchungu na maumivu katika usaliti wa mapenzi. Lavalava anaona hawezani wala hana bahati katika mapenzi. Ni wimbo ambao watu wengi waliweza kujihusisha nao na kufikia sasa una watazamaji zaidi ya milioni kumi.

https://www.youtube.com/watch?v=bmVXA2CXitI

Soma Pia: Nyimbo Tano za Rayvanny Zilizompa Umaarufu Bongo

Nitake Nini

Huu ni wimbo wake unaongazia kutoshelezwa katika upendo. Lavalava anaimba jinsi alivyompata mpenzi wa kweli, wa kumjali na kumsifia. Hivyo wimbo huu wenye mdundo wa pole pole ulipokelewa vizuri sana na kufikia sasa una watazamaji zaidi ya milioni tano nukta tano.

https://www.youtube.com/watch?v=iYAatHZ5pZI

Utatulia

‘Utatulia’ ni wimbo wa ahadi ya mapenzi ya milele. Lavalava anamsihi mpenzi wake amuambie iwapo atatulia kuwa na yeye. Ni wimbo ulikubaliwa na wengi kwa sababu ya ushahiri wake mzuri. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya milioni tano nukta mbili.

https://www.youtube.com/watch?v=gD0ZjiHSCOw

Bado sana

Wimbo huu ulitolewa siku chache kabla ya Mwaka Mpya na kwa sasa ni moja ya nyimbo kubwa nchini Tanzania. 'Bado Sana' ni wimbo unaonaangazia watu wenye majigambo wakidhani wamefaulu kushinda wengine, lakini jamii inafikiria vinginevyo. Kwenye YouTube, 'Bado Sana' inafanya vizuri sana na zaidi ya maoni Milioni tatu nukta tisa.

 https://www.youtube.com/watch?v=QN7o76eulRs

Leave your comment