Nyimbo Tano Kali Za Taarab Zinazovuma Bongo
25 January 2021
[Photo Credit: Leyla Rashid Instagram]
By Branice Nafula
Mziki wa taarab unaendelea kuwa kigezo cha kwanza katika kutambulisha mziki wa Tanzania barani Afrika. Mziki huo wenye ushairi wa michambo na hata maudhui ya mapenzi baado unaheshimika sana nchini humu.
Hadi sasa, mashabiki wa mziki wa taarab wanendelea kuupa mziki huo kipaumbele. Katika nakala hii tunaangazia nyimbo tano za taarab zinazovuma nchini Tanzania kufikia sasa:
Najiripua – Mzee Yusuf
Huu ulikua wimbo wake wa kwanza alipoamua kurudi mjini. Najiripua unazungumza juu ya mtu anayejitolea ili kumpenda mpenzi wake bila kujali watu wanasema nini. Huu ni wimbo ambao Mzee Yusuf aliachia mwaka uliopita na kufikia sasa umepata watazamaji zaidi ya laki nne.
Read Also: How Marioo Missed Out on Sho Madjozi’s ‘John Cena’ Hit
Mjini chuo kikuu – Khadija Kopa
Huu ni wimbo wake Khadija Kopa unaongazia namna mambo ya mjini ni magumu sana. Ni mahali ambapo watu wengi hupotea na pia mtu hujifunza kupambana na maisha kikamilifu. Wimbo huu uliwazingua wengi mwaka wa 2019 kwani maudhui yake yaliwagusa wengi kuhusiana na maisha ya mjini. Kufikia sasa ni wimbo wenye watazamaji zaidi ya laki mbili.
Mauzauza – Zuchu ft Khadija Kopa
Huu ni mojawapo ya nyimbo tano kwenye EP yake Zuchu. Zuchu alimshiriisha mamake Bi Khadija Kopa na ni wimbo wenye mdundo halisia wa taarab. Hivyo ushirikiano huu una michambo ya kuwakanya watu wenye hulka za kichawi na wivu. Ni wimbo wenye watazamaji zaidi ya millioni sita kufikia sasa.
Read Also: 5 Top 2021 Bongo Hits That Should be on Your Playlist
Ndo Yale Yale – Leyla Rashid
‘Ndo Yale Yale’ ni wimbo wa Taarab ambao unazungumza juu ya aina ya watu wasiopenda wengine kupendana na kuishi maisha mazuri. Kwa hivyo wimbo huonyesha ujumbe na kuelimisha jamii kuacha tabia kama hiyo.
Full Doz - Mzee Yusuf ft Leyla Rashid
Full Doz, ni wimbo wa Mzee Yussuf pamoja na Malkia wake Leyla Rashid. Wanazungumzia uzuri wa upendo, jinsi ya kumpenda na kumtendea mpenzi wako, na jinsi ya kuondoa uvumi.
Leave your comment