Kusah Aachia Wimbo Mpya kwa Jina ‘Mama Lao’

[Picha/Kusah Instagram]

Mwandishi Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii tajika wa mziki aina ya RnB Kusah ameachia wimbo mpya wa mapenzi kwa jina ‘Mama Lao’.

Huu ni wimbo Kusah aliuachia siku sawa na siku ya kumtambulisha mwanae na mwigizaji maarufu Auntie Ezekiel.

‘Mama Lao’ ni wimbo unaongazia namna Kusah anampenda mpenzi wake huku akielezea kwa nini huyo mpenzi ni ‘Mama Lao’.

Download Kusah Music For Free on Mdundo

Kusaah kwenye wimbo huu anasema mpenzi wake alitaka tu mapenzi ya dhati ila si pesa na yeye akampatia bila ya kufikiria mara nyingine. Anazidi kumuahidi mpenzi wake mapenzi hadi kifo kiwatenganishe.

“Yeye hakutaka pesa alitaka furaha, Nami nikampatia,Kwa yale madeko mtoto akaja Kusah nitakusalia, Unapokwenda nami nipo,Nimekubali yapitishwe maandiko,Imani yangu kwako ipo,Mimi nawe kitutenganishe kifo…” hii ni baadhi ya mistari kwenye wimbo huo.

Tukizingatia ushairi ulioko kwenye wimbo huu ni dhahiri kuwa Kusah alikua na lengo la kupasha ujumbe wa mapenzi bila ya kuficha lolote.

Soma Pia: Kusah Drops New Thanksgiving Song ‘Nilinde’ after Surviving Grisly Accident [Video]

‘Mama Lao’ ni wimbo unaoendelea kupaata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube na watazamaji zaidi ya elfu Ishirini na tisa.

Kufikia sasa wimbo huu bado huajatolewa video. Mdundo wa wimbo huu ulitengezwa na producer Gachi B.

‘Mama Lao’ ndio wimbo wa kwanza kutoka kwa Kusah mwaku huu wa 2021.

https://www.youtube.com/watch?app=desktop&v=PrICuNPYPFs&feature=youtu.be

 

Leave your comment