Harmonize Aachia Wimbo Mpya 'Anajikosha'

[Picha:BBC]

Mwandishi: Branice Nafula

Follow Us on Google News

Mkurungenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Anajikosha’.

‘Anajikosha’ ni wimbo unaoangazia wahusika wenye hulka potovu. Kimsingi Harmonize anawachambua watu wenye tabia ya kujigamba kwa vichache walivyonavyo.

Kwingineko ni kuwa mhusika huyo anaombwa ajaribu kujiheshimu kwa kiasi kwani tabia yake hiyo itakuja kumponza.

Harmonize anaanza wimbo huu kwa sauti yake nyororo na uzuri ni kuwa wimbo huu ni ushairi wa Kiswahili pekee.

“Jumamosi kakesha analewa Jumapili kanisani, anajikosha Eti sipendi vya kupewa Bango analipa shabani, anajikosha Shoga jana nilinoga Na nywele yako umetisha, anajikosha Nimesharudi naoga Jioni nitairudisha, anajikosha…” hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huo.

‘Anajikosha’ ni toleo la pili mwaka huu mpya kwa kazi yake Harmonize. Wimbo wake wa Kwanza mwaka 2021 ulikua ‘Wapo’.

Mdundo wa ‘Anajikosha’ ni wa kufurahisha kwani unampa mtu hamu ya kucheza wimbo mara kadhaa.

Soma Pia: Nyimbo 10 Bora Zilizotamba Bongo Mwaka wa 2020 [Video]

Kufikia sasa Harmonize hajaachia video za nyimbo zake mbili ila zinafanyavizuri kwenye mtandao wa YouTube.

‘Wapo’ inazaidi ya watazamaji milioni moja nukta tano huku ‘Anajikosha’ ina watazamaji zaidi ya laki mbili.

Kwingineko, Harmonize anatarajiwa kuwa na tamasha kubwa ndani ya hii miezi mitatu liitwalo “Indaclub Tour” ambapo atazunguka nchini Tanzania kufanya sherehe kubwa za mziki.

https://www.youtube.com/watch?v=PgAkMao0tEk

Leave your comment