Harmonize Asitisha Tamasha ya HarmoNight Iliyosubiriwa Sana

[Photo Credit:Harmonize Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Huku zikisalia siku chache kumaliza mwezi wa Novemba, mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize amelazimika kutangaza kuwa tamasha ya Harmonight imesitishwa.

Hii ilitarajiwa kuwa tamasha kubwa zaidi Tanzania mwisho wa mwezi huu. Akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alisema kuwa anasikitishwa sana kwani tamasha iliyokuwa inatarajiwa haitofanyika.

Download Harmonize Music for Free on Mdundo

“In so much tears to postpone my dream night hakuna nilichotakiwa nifanye na sijakifanya ili usiku huu utimie on behalf of @kondegang & @efmtanzania I'm giving you this sad news hapatokuwa na @harmonightcarnival 28/11/2020 Uhuru stadium kama tulivyo panga I don't even feel to explain more...!!! This…is hurting me. stay tuned for more,” aliandika Harmonize.

Soma Pia: Video 5 za Bongo Zinazotamba Mtandaoni YouTube

Haijabainika ni nini haswa kilichosababisha kusitishwa kwa tamasha hilo kubwa iliyofaa kuwa ya siku tatu mfululizo.

Hii ingekua show ya kihistoria katika tamasha zote za mziki nchini Tanzania. Wasanii mbali mbali walikua wanatarajiwa kuhudhuria and kutumbuiza wafuai wake Harmonize.

Kwa sasa, ni jambo la kusubiria uongozi wa Konde gang na washika dau wengine kutangaza tarehe mpya ya Tamasha hilo.

Kwingineko, Harmonize ametangaza kuwa amefunga mwaka na wimbo wake ‘Ushamba’.

Wafuasi wake wengi walikuwa na matumaini kuwa Harmonize ataachia albamu yake ya pili mwaka huu lakini hio ilisongeshwa mwaka ujao.

 Soma Pia: 5 TBT Bongo Videos That Can’t Age

Leave your comment