Rostam, Mr Blue Washirikiana Kuachia Wimbo Mpya 'Watani wa Jadi'

[Photo Credit:Rostam Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Wanamziki maarufu wa Hiphop kutoka Tanzania Rostam na Mr Blue wameshirikiana na kuachia wimbo mpya kwa jina “Watani wa Jadi”.

“Watani wa Jadi” ni wimbo unaoangazia timu mbili kubwa zenye mashabiki mahasimu tangia kitambo.

Wimbo huu “Watani wa Jadi” unazungumzi namna mashabiki wa timu ya Yanga na Simba FC wanapenda kutaniana na kuangazia namna timu zao ni bora kuliko zingine.

Stamina kwa upande wake anafungua semi za wimbo huu kama shabiki wa Yanga anapoelezea Mbona timu ya Simba si bora zaidi. Kwa upande wake, Roma aneleza mbona Simba ndio timu kubwa zaidi nchini Tanzania.

Download Roma Music for Free on Mdundo

“Mtakesha mkichoma ubani, mpandishe mashetani, mkija kanzu tobo, wayaaa, mpira kwapani sisi bingwa nyikani, watotowa jangwani labda aje simba wa jangwani…..Yanga Acheni usela, usela mavi vueni jersey vaeni dera litawapendeza hilo vazi….”

Kwingineko Sauti yake Mr. Blue inatambulika anapoimba kiitikio cha wimbo huu.

Wimbo huu unadhihirisha kuwa mashabiki wa timu ya Yanga na Simba wataendeleza utani wao wa jadi kwa muda mrefu zaidi.

Wimbo huu uliandaliwa na producer Bin Laden wa Tongwe records na mtayarishaji wa picha ni Nicklass.

Hivi karibuni wasanii wakubwa katika sanaa ya Bongo Harmonize na Diamond Platnumz walipata nafasi ya kutumbuuiza mashabiki wa timu wanaoshabikia wao wawili.

Diamond akiwatungia timu ya Simba Fc wimbo wa Singeli kwa jina “Simba” huku Harmonize akifanya vile na wimbo wa “Yanga”.

https://www.youtube.com/watch?v=yQh-Y-DSW9E&ab_channel=VIVAROMA

Leave your comment