Muigizaji H Baba Awashtumu Wasanii kwa Madai ya Kumshusha Nandy

[Photo Credit: Ralingo]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Muigizaji maarufu amewaponda wasanii wa Tanzania kwa kutaka kumshusha mwimbaji Nandy kwenye tasnia ya mziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram H Baba alindika ujumbe mrefu akizungumzia namna wasanii wacahache wanaharibu sanaa ya muziki wa Tanzania.

Kulingana na H Baba kuna kampeni za kumshusha Nandy ili msanii mwingine aoenekane mkubwa.

“Inasikitisha sana kama sanaa imefikia hapa tulipo kampeni kubwa iliopo nikumshusha Nandy ili nanii aonekane mkubwa atujakataa kwanini kina Nandy wasiwe 20 kina Kondeboy 40 ili tanzania ipepee nawaambia yule dada etu VANNESA nampa bigup sana kwa maamuzi aliyoyafanya japo atarudi kuimba akiwa amejipanga baada yakuwajua wabaya wake kwa upuuzi huu tunaoendelea kuukumbatia unaharibu sanaa ya Tanzania watu hawa ujifanya watu mbele yajamii kumbe koroboi tuu kwanini mpambane kumshusha mtanzania mwenyenu mnajiskiaje kuishusha sanaa ya Tanzania huku mkidanganya watu mmeipandisha sanaa hii nawaombeni sanaa niajira kubwa kwa kila mwanasanaa huu upuuzi unaoendelea nawaambia watu wakiujua wakatambua nia yenu niubinafsi muonekane nyinyi tuu wengine mnawashusha pia kuwatumia watu wawatukane ili wawashushe mnakosea mie situkani mtu naomba nieleweke,” aliandika kwa kifupi.

Mwigizaji huyu alikua makini kutotaja mtu yeyote ila alikua na ombi kwa wasanii wasaidiane kuipa Tanzania hadhii.

Alisisitiza kuwa ubinasfi kwenye sanaa ya muziki ndio chanzo cha michambo isiyo na faida kwa wasanii wa jumuiya ya Tanzania.

Download Nandy Music for Free on Mdundo

“Naokoa sanaa ya Tanzania kuondoa ubinafsi uliopo kwenye sanaa yetu #Ukimshusha Nandy unapata faida gani? Endeleeni ipo siku watanzania wataamka kupitia sanaa yao watawajua wabaya wa mafanikio ya sanaa yetu ya Tanzania inauma inaumiza inasikitisha vijana nitaifa la kesho Muacheni @officialnandy Wawatu nimwanamuziki aliekamilika uwezo mkubwa anapeperusha bendera ya Tanzania vyema uwezo unambeba watu utumia nguvu kubwa kushushana tuu sio kazi nzuri shindaneni kwa kazi nzuri sio kuzibiana njia kila msanii mzuri mkimshusha wakabaki wakwenu mnapata faida gani… H Baba alinakili.

Leave your comment