Hamisa Mobetto Kuachia Ngoma Mpya Hivi Karibuni

[Photo Credit:Hamisa Mobetto Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii kutoka Tanzania Hamisa Mobetto ametangaza kwamba hivi karibuni ataachia ngoma yake mpya.

Hii ni baada ya kutoachia mziki sasa kwa muda wa karibu mwaka mmoja.

Kwa sasa haijulikani ni lini wimbo huu utazinduliwa na inakisiwa kuwa Hamissa atamshirikisha msanii kutoka Nigeria.

Kwa upande wake Hamissa alitangaza hili kupitia mtandao wa Instagram na kuandika haya: “Guess who ….?Subscribe to my YouTube Channel (Hamisa Mobetto) Or you can just click the Link on My Bio…”

Kufikia sasa mashabiki wa Hamisa Mobetto wanaamini kuwa anayeshirikishwa kwa wimbo huo ni msanii kutoka Nigeria aitwaye Singah.

Singah ni mwanamziki anayejulikana kwa kufanya wimbo “Teyamo” uliompa nafasi ya kujilikana barani Afrika.

Miezi kadha iliypota, Hamisa alizindua tetesi baada ya kushirikishwa na Alikiba katika wimbo wake wa ‘Dodo’.

Katika ‘Dodo’ Hamisa alicheza sehemu ya mpenzi wa Alikiba ambapa walifanya harusi. Video ile ilileta tetesi sana wengi wakimkera Hamisa kwa kukubali kushirikishwa ilhali yeye na Diamons wana motto pamoja, na Diamond na Alikiba hawana uhusioano mzuri.

 

Leave your comment