Joh Makini Afungua Lebo Mpya na Kuzindua Msanii wake wa Kwanza

[Photo Credit: Joh Makini Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Mwanamziki  Joh Makini ametangaza kufungua lebo yake mpya. Makini ni msanii mkubwa wa mziki aina ya Hip-hop, ambao unaendelea kupata umaarufu zaidi nchini Tanzania.

Katika  hafla na wanahabari Makini alisema amefunga lebo kwa jina Makini Records ambayo itaweza kuwasajili wasanii wenye vipaji .

“Makini Records ni recording  label ya Joh Makini amabayo tunaizindua leo, ambayo sasa tutakua na uwezo wa kuwasaidia officially wasanii ambao wana uwezo mkubwa wa kufanya mziki kubadilisha maisha yao, malengo makubwa ya Makini records ni kuhakikisha tunatengeza vipaji vinakua na uwezo wa kudumu……” Makini alisema. 

Katika hafla hio, Makini alimtambulisha msanii wake wa kwanza aitwaye  Otuck William. Kufikia sasa Otuk William ashazindua ngoma yake ya kwanza chini ya lebo ya Makini Records iitwayo ‘Mbele kwa Mbele’.

‘Mbele kwa mbele’ ni wimbo wa mapenzi ambapo Otuck anamwimbia mpenzi wake kuwa mapenzi yao yatendeleea kuenda “Mbele kwa mbele”.

Wimbo huu umeendaliwa na director Ivan kutoka Tanzania. Video yenyewe pia ina uzuri wake  kuanzia kwa ubunifu hadi mavazi . 

Makini ni mojawapo wa wasanii  kutoka kundi la Hiphop la Weusi . Anatambulika kama moja wapo wa magwiji kwenye tasnia ya  Hiphop.

Makini amefanya kazi mingi za mziki pamoja na collabo kadhaa ambazo zimempa hadhi katika sanaa ya mziki.

https://www.youtube.com/watch?v=W1qxgiUBqRk&ab_channel=OtuckWilliam

Leave your comment