Jux Arejea na Wimbo Mpya wa Mapenzi ‘Sio Mbaya’

[Photo Credit: Juma Jux Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Mwanamziki wa Tanzania Juma Jux amezindua wimbo wake mpya kwa jina ‘Sio Mbaya’.

‘Sio Mbaya’ ni wimbo wa mapenzi unaongazia watu wawili walopendapana hapo awali japo waliachana.

Katika wimbo huu tunaona wanawake wawili wakizozana kwa ajili ya mwanamme wanaompenda

Katika ‘Sio Mbaya’, Jux anaangazia vile mapenzi yao ya awali yalivyoharibika akisisitiza kuwa yule mrembo ndiye aliamua kumuacha ila bado yeye anampenda hivyo basi akihitaji kumuongelesha yeye kaona ‘Sio Mbaya’.

“Kwa nini ukiniona, Unakosa furaha, Si acha kuna kuna, Kwa nini ujipe karaha mama, Mi najua unachotaka wee, Unachowazaga, Ata mimi napitiaga, Ila tunajikaza eeh, Na siwezi kumaliza verse Bila kusifia your pretty face, Machoni mwako naona loneliness, Loneliness….” hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huu.

Download Jux Music For Free on Mdundo

Kwenye video, Jux alifan kazi nzuri katika kuangazia mapenzi hayo. Jux ameiachia nyimbo hii wakati amabapo wasanii wengi wa Tanzania wanaendelea kufanya vizuri katika muziki hata baada ya janga la Corona kusitisha tamasha za kimataifa.

“Sio Mbaya” imetengezwa na director Ivan. Kwenye mtandao wa YouTube wimbo huu wa ‘Sio Mbaya’ inaendelea kupata umaarufu zaidi na watazamaji za elfu 47. Hii ni hakikisho kuwa Jux ana weledi katika fani ya mziki wa bongo hasa RnB.

https://www.youtube.com/watch?v=lMlwunll7OQ&ab_channel=AfricanBOY

Leave your comment