Harmonize Aalikwa Ikulu ya Tanzania Baada ya Wimbo Wake Maarufu ‘Magufuli’

By Rodgers Omondi

Mwanamuziki tajika nchini Tanzania Harmonize ametoa shukrani zake kwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kumualika katika ikulu jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alieleza kwamba alipata nafasi ya kujumuika pamoja na rais Magufuli, rais mstaafu Jakaya Kikwete na viongozi wengine mashuhuri.

Jana Nilipata Nafasi Ya Kujumuika Katika Dhifa Ya Taifa Ilioandilia Na Raisi Wetu Kipenzi Doctor John Pombe Magufuli statehouse Jijini Dar es salaam Naamini Nilikuwa Pale Kuwakilisha Vijana Wengi Walio Mtaani Na Wenye Ndoto...!!! 

“Hakika ilikuwa Bahati Kwangu Kukutana Na Viongozi Wa Ngazi Za Juu Kabisa Kila Nilie kutana Nae Pale Ndani Alinipongeza Sana..!! Na Kuniambia wanajivunia Uwepo Wangu Katika Hili Taifa Tukufu Ilinipa Moyo Na Somo La Kwamba Kupitia Kipaji Chako Au Kazi Yako Hiyo Hiyo ifanye Kwabidi...!!! 

“Utatimiza Kila Aina Ya Ndoto Yako...!!! Na Kupewa Kila Aina Ya Heshima..!! Kijana Mwenzangu Chukua Hiyo Lakini Mwishoni Kabisa Nikakutana Na Swahiba former President D.R Jakaya Mrisho Kikwete Tulifurahi Sanaa Akaniambia Wewe Sasahivi Sio Msani Tena Wewe Ni Mwanamuziki Ni Wakati Wa Kuifanya Tanzania Iendele Kuwa proud Na Wewe Watanzania Woteeee Wanakupenda Na Wana kusupport Go go go.....!!!” Harmonize aliandika kwenye ukurasa wake.

Wiki mbili iliopita, mwanamuziki huyo alitoa wimbo ‘Magufuli’ ambao unamsifu Rais Magufuli pamoja na uongozi wake.

https://www.youtube.com/watch?v=FrAZ5Lzf5AU

Leave your comment

Other news