Ommy Dimpoz Aeleza Alivyokata Tamaa ya Kuishi

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amebainisha kuwa alipokuwa kwenye matibabu nchini Ujerumani alikata tamaa na kudhani angepoteza maisha baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Ommy Dimpoz amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya koo kwa muda mrefu baada ya kusemekana kula chakula chenye sumu, hali ambayo ilimfanya afanyiwe upasuaji Afrika Kusini.

"Nilifanyiwa operesheni kwa masaa manane, na nilipofika Ujerumani nilifanyiwa upasuaji na madaktari wa kijerumani wengi zaidi ukilinganisha na Afrika Kusini", amesema.

Some mengi: EATV

Leave your comment

Other news