Rayvanny Atoa Wito Kwa Wasanii ‘Kidogo Tunachopata, Tusaidie Ndugu Zetu Wenye Magonjwa’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka WCB, Rayvanny amewataka Watanzania wenye uwezo kwajitoe japo kidogo kuwasaidia wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali Hospitalini.

Rayvanny amesema hayo, baada ya jana kutembelea katika Hospitali ya Muhimbili kumjulia hali mama aliyekuwa anasumbuliwa na jicho kutoka Mbeya, ambaye wiki iliyopita video zake zilisambaa mtandaoni zikimuonesha akiomba msaada wa matibabu.

Rayvanny ndiye aliyeanza kutoa taarifa za mama huyo aliyekuwa anasumbuliwa na jicho na tayari ameshapatiwa matibabu siku ya jana.

This article was originally published by bongo5.com

Leave your comment