Victoria Kimani Afananishwa na Nicki Minaj Nchini Ufaransa, Wadau Wamsimamisha na Kuomba Picha

Je, ni kweli kuwa mrembo kutoka Kenya, Victoria Kimani ambaye pia ni msanii wa muziki nchini humo anafanana na rapper Nicki Minaj wa kutoka Marekani? hilo nakuachia ujaji mwenyewe.

Victoria Kimani kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema kuwa alipokuwa Ufaransa alifananishwa na wanandoa wawili ambao walimuomba apige picha na mtoto wao.

Hata hivyo, Kimani amedai kuwa hakuwambia kama yeye sio Nikki Minaj bali alikubali kupiga picha na mtoto wao na kisha kuendelea na safari yake.

This article was originally published by: bongo5.com

Leave your comment