TANZANIA: Alikiba Afunguka Sababu ya Kufuta Wimbo

Msanii wa muziki wa bongo fleva Alikiba ambaye hivi karibuni amekumbana na lawama na kejeli za mashabiki baada ya kufuta wimbo wake mpya wa 'hela', amefunguka sababu za kufuta wimbo huo uliomuweka pabaya.

Akizungumza na kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Alikiba amesema sababu kubwa ya kufuta wimbo huo ni siku ambayo aliachia, kwani haikuwa siku ambayo huitumia kuachia nyimbo mpya.

“Siku yenyewe haikuwa siku yangu ambayo napenda kurelease nyimbo, ilikuwa siku ya Jumanne so tukamwambia jamaa autoe, inatakiwa siku kama ya leo Alhamisi, ndio maana ulikuta umetoka kwenye Youtube, ila sasa hivi ukiingia utaikuta”, amesema Alikiba.

Alikiba amelazimika kutoa maelezo hayo baada ya kushambuliwa na mashabiki kuwa ameutoa wimbo huo kwa kuwa ni mbaya na wa zamani.

Source: eatv.tv

Leave your comment