TANZANIA: Darassa Azigomea Milioni 9

Mkali wa Hip Hop Darassa, ambaye mwaka 2017 alitamba na Hit zake kadhaa ikiwemo, Kama Utanipenda, Muziki na Too Much huku hivi sasa akiwa hasikiki, meneja wa Juma Nature na msanii wa zamani Rich One amesema aliwahi kumpa dili la milioni 9 lakini akakataa.

Rich One ambaye leo alikuwa kwenye Heshima ya Bongofleva ya Planet Bongo ya East Africa Radio, ameweka wazi hilo kuwa dili hiyo ilikuwa ni sehemu ya dili mbalimbali ambazo huwa anawapa wasanii.

''Wasanii wengi sana nawapa dili kupitia udalali wangu, napata simu nyingi za 'show' mikoani nawaunganisha na nimewahi kumpa dili Darassa wakati anatamba nilipigiwa simu ya 'show' ya milioni 9 lakini akaikataa akawa anataka milioni 15'', amesema Rich One.

Rich One amekiri kuwa hawezi kumlaumu Darassa kwani alikuwa kwenye wakati wake lazima angetaka kupata nyingi zaidi japokuwa mambo hayakwenda vizuri hadi sasa hasikiki.

Rich One ambaye alitamba kitambo enzi hizo na kundi la TMK Wanaume na baadaye Wanaume Halisi, kwasasa amesema anasimamia kazi za Juma Nature huku akiendelea na kazi yake ya msingi ambayo ni udalali.

Source: eatv.tv

Leave your comment