CONGO: Koffi Olomide Kukamatwa Zambia

Picture/ courtesy

Mwimbaji Staa kutokea Congo DRC Koffi Olomide amepigwa stop kuingia kwenye taifa la Zambia baada ya shutuma za kumshambulia Mwandishi mpiga picha mara ya mwisho alipokuwepo kwenye taifa hilo.

Tuhuma nyingine alizonazo huko Ufaransa za kuwanyanyasa kingono Dancers wake, kuwateka na kuwaajiri bila vibali zimechangia pia kupigwa hiyo stop na Zambia ambapo Ubalozi wa Ufaransa Zambia siku ya jumamosi ulisema Koffi Olomide akiingia Zambia akamatwe.

kwa mujibu wa BBC na Mwandishi wake Kennedy GondweKoffi Olomide mwenye umri wa miaka 62 ambae anaishi Congo DRC alitakiwa kutumbuiza kwenye matamasha mawili nchini Zambia mwezi huu lakini Serikali ya nchi hiyo imesema atakamatwa pindi tu atakapokanyaga kwenye ardhi hiyo.

Koffi mwenyewe amenukuliwa akisema kwamba Zambia ni nyumbani kwake pa pili na anapenda Wanawake wa Zambia, vilevile angependelea kutumbuiza tena siku moja kabla hajafa.

Hii sio mara ya kwanza kwa Koffi kujikuta matatizoni, mwaka 2016 alinaswa kwenye camera akimpiga dancer wake wa kike wakati wakiwasili Kenya, tukio hilo likamfanya aondolewe nchini humo pamoja na Wakenya kumuwakia kwa kitendo hicho cha kikatili.

2008 aliingia matatizoni kwa tuhuma za kumpiga cameraman wa TV binafsi ya congo na kuvunja kamera yake kwenye tamasha mjini Kinshasa baada ya kutoelewana kuhusu haki za kurekodiwa, mwaka 2012 pia alijikuta matatizoni kwa kukutwa na hatia ya kumshambulia Producer wake Diego Lubaki.

Source: millardayo.com

Leave your comment

Other news