TANZANIA: MFALME WA MUZIKI NI NANI? DIAMOND PLATNUMZ AU ALIKIBA?

Muziki ndio mfalme wa muziki. Ndio sababu wasanii wa muziki wanajitahidi kuufanyia kazi muziki ili uwe bora na mkubwa zaidi. Wanamuziki ni vibarua wa muziki. Muziki hauwezi kutawaliwa na wasanii bali wasanii hutawaliwa na muziki na ndio maana muziki utabakia kuwa muziki hata wanamuziki wakubwa wakichujuka sokoni. Hakuna msanii anayestahili kuitwa eti mfalme wa muziki wakati anahangaika kufanya kazi zake ili kubaki kwenye ufalme wa muziki. Muziki utaendelea kuwa mkubwa bila kujali majina ya wanamuzi wakubwa yanavyotoweka na kuja mengine.
Muziki mfalme daima.
Imeandikwa na Kaka Dani wa www.facebook.com/kakamtuhuru

Leave your comment

Other news