TANZANIA: Joh Makini Ataja Kolabo Tatu Za Kimataifa Alizonazo

Rapper kutokea kundi la Weusi, Joh Makini ameweka wazi idadi ya kolabo za kimataifa alizonazo kwa sasa.

Joh Makini ameeleza kuwa hadi sasa kolabo ambazo anaweza kuziweka wazi na kuzizungumzia ni tatu.

“So far International collabo ambazo naweza kuzizungumzia ambazo zipo ni mimi na Fallz, Y CEE,Cassper Nyovest ambayo watu wameisikia nipo katika kuangalia uwezekano wa kufanya ngoma nyingine naye,” Joh Makini ameiambia Bongo5.

Kwa upande wa kundi la Weusi, Joh Makini amesema tayari wamesharekodi nyimbo mbili na kundi la Sauti Soul kutokea nchini Kenya ila zimekataa muda studio hivyo wanaangalia kama wanaweza kurudia kurekodi upya ili kuweza kuendana na wakati wa sasa.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news