TANZANIA: P The MC Kuja Kivingine, Albamu Mkononi

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, P The MC amefunguka sababu za ukimya wake kimuziki.

Rapper huyo kutoka kundi la SSK ameeleza kuwa kwa sasa amekamilisha kurekodi albamu yake ambayo kazi kubwa imefanywa na producer Cjamoker ingawa kuna nyimbo zimefanyika na S2kizzy.

“Nilichukua muda kufuatilia kujifunza muziki, how to be close to my fans na ni wafanyie vitu vya aina gani ili niweze kukidhi kiu ya mahitaji yao na baada ya kushughulikia hilo nikaingia studio kusimamia albamu,” P Th MC ameiambia Bongo5.

Ameongeza kuwa kila wimbo utakao kuwa ukitoka katika albamu hiyo utakuwa ukitoka pamoja na video yake. Wimbo wa mwisho kwa P The MC kutoa rasmi unakwenda kwa jina la Mitaa Nayotoka.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news