TANZANIA: Nahreel Aangukia Mikononi Mwa Akon na Kery Hilson

Ukitaja waandaaji wa muziki waliofanya ngoma kubwa nchini Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo huwezi kuuacha kumtaja Nahreel kutoka studio za The Industry.

Sasa ukweli ni kwamba licha ya kufanya ngoma nyingi za wasanii wakubwa barani Afrika akiwemo Mr. Eazi na Patoranking, tayari mkali huyo wa midundo ameshafanya kazi na Akon na Kery Hilson.

Akithibitisha taarifa hizo memba mwenzie wa kundi la Navy Kenzo, Aika amesema kuwa tayari Nahreel ameshamaliza kufanya kazi hizo na kinachosubiriwa ni muda tu.

"Kuna meneja wetu mmoja nchini Marekani ambaye amejaribu kumfanya Nahreel afanye kazi na Akon.. na Kery Hilson soo! Nahreel soon anafanya nao kazi," amesema Aika kwenye mahojiano yao na Times FM kwenye kipindi cha Playlist.

Source: bongo5.com

Leave your comment