TANZANIA: Navy Kenzo Waweka Wazi Mipango ya Kufunga Ndoa

Wasanii Nahreel na Aika wanaounda kundi la Navy Kenzo ambao pia ni wapenzi wamefunguka kuhusu mipango ya kufunga ndoa.

Nahreel ambaye ni producer pia katika mahojiano na FNL ya EATV alieleza kuwa muunganiko wao kama wapenzi ni muhimu zaidi kwa sasa kabla ya ndoa.

“Mimi na Aika nadhani the bond ni special, wedding ni important kufanyika katika maisha lakini Bond yangu na Aika is very special,” alisema Nahreel.

Kwa upande wake Aika alieleza kuwa; ‘Na tusiwafundishe watu wengine kuwa walazimishe kuingia kwenye ndoa kabla mtu hajawa tayari kuwa na ile bond, ni muhimu sana’.

Navy Kenzo ambao wanatamba na ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la Fella, katika mahusiano yao ambayo yamedumu kwa takribani miaka 10 sasa wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume.

Source: bongo5.com

Leave your comment