TANZANIA: Ben Pol Kufanya Ngoma ya Kihistoria, Kukutanisha Wasanii 11

Wakati Ben Pol akiendelea kufanya vizuri na ngoma yake ‘Bado’ kidogo, muimbaji huyo yupo mbioni kuachia remix ya ngoma hiyo kwa kuwakutanisha wasanii 11.

Wasanii ambao watakuwepo katika ngoma hiyo ni pamoja na Vanessa Mdee, Joh Makini, Willy Paul, Roma, Bill Nass, Fid Q, Barnaba, Nandy Wyse na Jux.

Ngoma hiyo ambayo bado hajajulikana ni siku gani hasa itatoka, mkono wa producer Tiddy Hotter ndio umehusika ila Mixed na Mastered amefanya Mona Gangster.

Bado Kidogo original version ilitoka January 2 mwaka huu na hadi sasa ina views  396,574 katika mtandao ya YouTube.

Ni kipindi kirefu Bongo Flava hajashuhudia ngoma zikifanyiwa remix na kushirikisha idadi kubwa ya wasanii, miongoni mwa ngoma zilizowahi kukutanisha wasanii wengi ni Mchizi Wangu Remix ya Nako 2 Nako Soldiers na Hapo Vipi Hapo Sawa Remix ya Prof Jay.

Courtesy: bongo5.com

Leave your comment