UGANDA: “Nimefanya Wimbo na Radio, Tulikuwa Tunajiandaa Kushoot Video” - Vanessa Mdee

Mwimbaji Staa wa Bongofleva Vanessa Mdee ambaye kwa sasa yupo nchini Nigeria katika ziara yake ya kimuziki kwa ajili ya kutambulisha album yake ya Money Mondays amemzungumzia marehemu Radio ambaye hivi karibuni alipost picha wakiwa pamoja kumbe ilikuwa ni ishu ya wimbo walioufanya.

Vanessa amesema kuwa walikuwa kwenye mipango ya kushoot video ya wimbo huo na walikuwa wanamawasiliano mpaka alipopata ajali.

Pia ameeleza jinsi alivyopokea taarifa za msiba kwa mshtuko kwani mara ya mwisho aliwasiliana na Weasel kupitia simu ya Radio kipindi akiwa amelazwa na alipanga kwenda kumuona kipindi akirudi kutoka Lagos Nigeria lakini ndipo ikatokea amefariki.

Source: millardayo.com

Leave your comment

Other news