TANZANIA: Vanessa Mdee Asema Wasanii wa Bongo Wanaosikika Nigeria ni Yeye na Diamond Pekee

Msanii wa muziki Bongo, Vanessa Mdee amesema muziki wa Afrika Mashariki haupewi nafasi kubwa nchini Nigeria kama inavyokuwa ikitazamiwa.

Muimbaji huyo ambaye yupo nchini humo kwa ajili ya kutangaza albamu yake ‘Money Mondays’ ameiambia Clouds Fm kuwa katika moja club alizopita alikuta ngoma zinazochezwa ni ya Patoranking na Diamond ‘Love You Die’ na ile aliyoshirikiana na Reekado ‘Move’.

“Hapa Nigeria haupo kabisa muziki wa Tanzania, haupo kwa nguvu ambayo unatakiwa kuwepo kwa sababu tunaelewa muziki wetu ni mkali, wasaniii wetu ni wakali. Kidogo wanauzito wa kupokea muziki wa East Africa, jana nilikuwa club nilisiki nyimbo za Tanzania ambazo zinapigwa ni ile Diamond na Patoranking na ya kwangu  na Reekado ‘Move’ hakuna nyimbo nyingine inapigwa hata ya Afrika Mashariki,” amesema.

Pia Vanessa amesema si kwamba hawatambui muziki kutoka Afrika Mashariki ni mzuri ila wameamua kuupa kipaumbele muziki wao na kutokana na idadi kuwa wasanii walionao inakuwa ni vigumu kwa muziki kutoka sehemu nyingine kupata nafasi.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news