TANZANIA: Ngoma ‘Wowowo’ ya ZaiiD Yajiwekea Rekodi

Ngoma ‘Wowowo’ kutoka kwa rapper ZaiiD ambayo imekamata mtaa vilivyo imejiwekea rekodi ya aina yake kwa msanii huyo na muziki wa hip hop Bongo kwa ujumla.

Wowowo imekuwa ni ngoma ya kwanza kwa ZaiiD kufikishwa views milioni moja katika mtandao wa YouTube. Akizungumzia hatua hiyo ZaiiD amesema hiyo ni hatua kubwa kwake na asingependa kuona anarudi nyuma.

“Binafsi nahisi kama ni ushindi kwa sababu sijawahi hata kufikisha hizo laki tano, na niseme tu kwa niaba ya watu wa hip hop kwa sababu video nyingi za hip hop zilizofikisha milioni zinaweza zisifike hata tano kwa Tanzania nzima, kwa hiyo binafsi naona ni ushindi mkubwa kwangu na ni hatua kubwa nimeifungua ambayo sitataka ifunge tena,” ZaiiD ameiambia Bongo5.

ZaiiD ameongeza kuwa kilichofanya ngoma hiyo kupendwa na wengi ni ubunifu ingawa mwanzo alipata upinzani hasa alipokuwa akipeleka video yake katika tv station lakini watu ameipokea kitu ambacho anaamini kwake ni nguvu ya umma.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news