"Hakuna wa Kunitisha" - Bright

Msanii chipukizi wa bongo fleva mwenye 'hit song ya Sina' Bright ameibuka na kujigamba kwamba hakuna mwanamuziki yeyote anayeweza kumhofia katika utendaji wake wa kazi kwa madai muziki wake una uwanja mpana.

Bright amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa 'East Afrika Television' baada ya kuwepo minong'ono mingi ya chini kwa chini kuwa wasanii wengi wanaochipukia wanashindwa kufanya vizuri katika kazi zao kwa kuhofia uwepo wa Aslay kutoka na kazi zake anazoziachia mara kwa mara.

"Mimi napambana na yeyote ambae anafanya vizuri katika 'game', kwa sababu muziki wangu una uwanja mpana na kila mtu anafahamu Bright anafanya kitu gani na sijawahi kuwa na 'stress' za mtu yeyote katika hii 'game', kwa sababu mimi ninachokifanya ninakiamini pia nashukuru ninachofanya kina kubarika watu wana-support mimi naendelea kufanya kazi bora kila siku",alisema Bright.

Kwa upande mwingine, Bright amesema anawashukuru mashabiki zake kwa kuipokea vizuri kazi mpya ya sina huku akiwaahidi kuendelea kuwapa vibao vikali kila baada ya miezi mitatu kutoka sasa.

Source: eatv.tv

Leave your comment