TANZANIA: Sababu ya Nandy Kuandika ‘Kivuruge’

 

Msanii Nandy ambaye siku chache zilizopita ameshinda tuzo ya AFRIMA za nchini Nigeria, ameeleza maana ya ngoma yake mpya ‘Kivuruge’.

Ngoma hiyo ambayo imetayarishwa na Kenny Ringtone, Nandy amesema amelenga kuzungumzia mwanamke aliye katika mahusiano lakini kuna vitu vimemchosha hivyo anataka kuondoka.

“Nimezungumzia mapenzi kwa upande wa mwanamke kuzungumzia mwanaume japo ni wimbo ambao unaweza kutumika kwa pande zote mbili, nimebeba uhusika wa mwanamke kwa mimi ni mwanamke pia” amesema Nandy.

“Ni maumivu ya mapenzi mwanamke analalamika kwa wanaume wake kuna kitu amemfanyia lakini so far anahitaji amuache kwa sababu anaamini taratibu maamuivu yake yataisha taratibu” ameongeza.

Nandy ambaye bado anafanya vizuri na ngoma ‘Wasikudanganye’, pia hivi karibu alitoa ngoma iliyokwenda kwa jina Mahabuba ambayo amemshirikisha Aslay.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news