NEW MUSIC: Ben Pol Kuachia Video Ya ‘Tatu’ Soon

Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol ameeleza ni kwa nini hadi sasa video ya wimbo wake mpya ‘Tatu’ aliomshirikisha Darassa haijatoka.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Show Time cha Radio Free Africa, kuwa hawakutaka kutoa video ya wimbo huo kipindi cha Mfungo wa Ramadhan, ingawa hadi sasa imeshakamilika.

“Video ya tatu imeshaisha na tayari ninayo, video imeshashutiwa na nipo nayo hapa ndani zaidi ya wiki moja na nusu sasa, naiangalia naonesha na watu, Sema tu kwenye time ndio tunaangalia tutoa muda gani kwa sababu hatukutaka kutoa kati kati ya Ramadhani, kwa hiyo mwishoni mwa mwezi wa Ramadhan itatoka,” amesema Ben Pol.

Source: bongo5.com

Leave your comment