Timmy Tdat na Sudi Boy Wafunguka Kuhusu ‘Zile Mbili’

Timmy Tdat kutoka lebo ya Kaka Empire inayoongozwa na King Kaka, amefunguka kuhusu wimbo wake mpya ‘Zile Mbili’ aliomshirikisha Sudi Boy.

Ahkiongea na Bongo5, muimbaji huyo wa Kenya amesema, “Nimefanya kazi na Sudi Boy kabla na mimi nilipenda kazi yake, ubunifu na nguvu, hivyo ilikuwa rahisi kufanya tena kazi pamoja naye kwenye Zile Mbili,” amesema Tdat.

Naye Sudi amefunguka kuhusu wimbo huo kwa kusema, “Zile Mbili ilikuja wakati tulikuwa kwa birthday ya jamaa flani, ikaja tu kama chorus ndio tukaamua kuingia studio. Napenda sana kazi ya Timmy Tdat. Tunayo chemistry ambayo inaingiana poa.”

Wimbo huo umetayarishwa na Bizzy B huku video yake ikiongozwa na Enos Olik. Tazama video hiyo hapa chini.

https://youtu.be/LYAi8fA0xH4

Source:bongo5.com

 

Download 'Zile Mbili' on Mdundo

Leave your comment