TANZANIA: Dayna Nyange Ang’ara Katika Tuzo za BEA, Nigeria 2017

Msanii wa muziki nchini anayefanya vizuri na wimbo ‘Komela’ Dayna Nyange amechukua tuzo mbili za BEA nchini Nigeria zilizotolewa weekend iliyopita.

Muimbaji huyo amechua tuzo ya Best African Artist pamoja na Best Vocal Performance Female.

Dayna ameiambia Bongo5 kuwa kamati ya tuzo hizo inafanya mchakato wa kumtumia tuzo zake.

Kupitia Instagram ameandika:

Leo imekuwa siku yangu ya furaha sana sana sana Na ningependa ni washukuru woteeMliokesha mkiniombea, mlikesha mkihamasisha, mlikesha mkinipigia kura. Hatimaye tumefanikiwa kutwaa tuzo zote mbili nchini Nigeria.
BEST VOCAL PERFORMANCE FEMALE
BEST AFRICAN ARTISTE
Ahsanteni sana mashabiki zangu , ahsanteni sana Wadau wangu, ahsanteni sana Media zote, watangazaji, waandishi, na ma dj. Ahsante sana producer wangu Mr.Ttouch, shukrani kwa menejiment yangu na wasanii wenzangu.
Sote tuliacha kazi na tukafanya kazi moja tu na hatimaye Matunda ni haya.Sijashinda mimi tu @daynanyange bali imeshibda Tanzania na Afrika kwa ujumla
#JuhudiZimezaaMatunda Mungu awabariki sana.

Source: bongo5.com

Leave your comment