TANZANIA: Bill Nass Akiri Kuwa Chorus ya Nazizi Kwenye Raha Ndio Ilimweka Kwenye Ramani ya Muziki

Rapper Bill Nass hawezi kusahau mchango mkubwa wa Nazizi na TID kwenye maisha yake ya muziki.

Wawili hao waliufanya wimbo wake uliomtoa, Raha uwe na mvuto mkubwa.

Akimpongeza Nazizi kwenye siku yake ya kuzaliwa wiki hii, Bill ameielezea chorus iliyofanywa na muimbaji huyo wa kundi la Necessary Noise kuwa ndio ilikuwa kila kitu.

“Nakutakia maisha maref miaka mobb momma wa taifa,” aliandika Bill Nenga.

“U know I love u….!!have a blast chorus yako ndo imefanya leo wananiita Nenga mara Mzungu Mzee nabado nakomaa tuu….hope ur very proud too….hbd @nazizihirji.

Raha ndio wimbo uliomfanya rapper huyo atajwe kuwania tuzo za KTMA kwenye kipengele msanii bora chipukizi miaka miwili iliyopita.

Source: bongo5.com

Leave your comment