TANZANIA: Inawezekana Wasanii wa Kike Hatupendani - Maua

 

Baada ya kuwepo tetesi za wasanii wa kike kubaniana nafasi, Maua Sama amefunguka na kudai hayo ni maneno ambayo yapo na hayakwepeki kwa sababu watu wamekariri kwa kusikia zaidi kuliko kufanya utafiti.

Maua amesema kuwa tetesi hizo hazina tofauti na zile ambazo wanawake husema wanaume wote ni sawa na kuongeza kwamba yeye hajawahi kukutana na changamoto hizo kwa kuwa kila alipoenda kuhitaji ushirikiano na watoto wa kike alipatiwa.

Aidha Sama ameongeza kuwa lisemwalo linawezekana likawepo lakini kwa vile yeye si muathirika wa matendo hayo ndiyo maana anashindwa kuweka bayana.

“Inawezekana kweli wanawake hatupendani, siwezi kumuongelea kila mmoja mimi binafsi sijawahi kupata changamoto hiyo na hata baadhi ya wasanii waliohitaji msaada wangu huwa wanaupata haraka kwa sababu mimi ni mtu wa upendo ndiyo maana nadhani na mimi huwa wananirudishia fadhila” – Maua Sama.

Maua ameongeza kuwa watu wengi wanashindwa kumkariri katika nyimbo zake kwa kuwa tayari ni utaratibu aliokwisha kuuweka tangu mwanzo wa kubadilisha ladha ya muziki ili aendelee kusimama imara katika muziki.

Source: eatv.tv

Leave your comment