Willy Paul Aelezea Kwa Nini Diamond ni Role Model Wake

Msanii maarufu wa muziki wa gospel nchini Kenya, Will Paul kwa miaka mingi amekuwa akionesha kupenda kile anachokifanya Diamond Platnumz kiasi cha kujiongezea jina Msafi.

Nimezungumza naye na kumuuliza kwanini anamchukulia Diamond kama role model wake.

“Muziki wa Diamond kuanzia kitambo, mavazi, lifestyle and then he is very hardworking artist, cause I think mimi nimekuwa nikimfollow I think for almost six years sasa,” anasema Willy.

“Wengi wanaongea hawajui mimi lini nilianza kumwangalia na hawajui naangalia Diamond kwanini. Cause nimeona hustle yake.”

Huko nyuma Willy alikuwa amepanga kumshirikisha Diamond kwenye moja ya nyimbo zake lakini haikuwa rahisi kutokana na masuala ya dini lakini sasa anasema kuna uwezakano huo.

“Hiyo ilikuwa imeleta issue lakini sasa unajua mimi nashukuru Mungu place vitu vimefikia saa hii at least now we can work. We had a meeting yesterday, a very fruitful meeting, so we thank God for everything,” amesisitiza.

Willy Paul yupo Dar es Salaam kwenye ziara ya vyombo vya habari kupromote wimbo wake mpya I Do aliomshirikisha msanii wa Jamaica, Alaine.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news