KENYA: Willy Paul Aweka Rekodi Hii Kwenye Muziki wa Kenya

Msanii wa nyimbo za kumtukuza Mwenyezi Mungu Willy Paul Msafi wiki hii ameweka historia ya kipekee sio tu katika muziki wake ila pia katika kiwanda cha muziki nchini Kenya.

Naam, kuna msemo unaosema kuwa atafutaye hachoki na labda huchoka akishapata anachosaka. Baada ya Willy kuweka nguvu nyingi katika kutengeneza kiki ambapo alifikia hatua ya kuwadanganya raia kuwa wapo katika uhusiano wa kimapenzi na mdada huyo, hatimaye jitihada zake zimeonekana kuleta mafanikio katika muziki wake kwa kuwa msanii wa kwanza wa muziki nchini kuwahi kufikisha idadi ya watazamaji milioni moja ndani ya wiki moja kwenye mtandao wa YouTube kupitia wimbo ‘Yes I do’ aliyomshirikisha msanii wa Jamaica Alaine.

Kabla ya Willy Paul kufanya hivi, nafasi hii ilikuwa ikishikiliwa na Nyashinski ambaye alifanya comeback ya nguvu kwenye game mwaka jana na nyimbo; ‘Now You know’ na ‘Mungu Pekee’.

Nampongeza sana Willy Paul kwa hatua anayozidi kupiga kwenye hii sana inayoifanya japo wakati mwingine safari inakuwa sio rahisi. Cha msingi ni kufanya unachokipenda kwa njia nzuri na sawa.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news