TANZANIA: Mwacheni Harmorapa Ajitapatie Riziki Yake - Diamond

Harmorapa limekuwa jina tajika kwa sasa si nchini Tanzania pekee bali tayari limeanza kupenya eneo zima la Afrika Mashariki. Mkali huyo kwa sasa anatamba na wimbo Kiboko ya Mabishoo aliyoifanya hivi karibuni akimshirikisha mkongwe wa Bongo flava Juma Nature aka Sir Nature.

Kama utani tu, rapper huyu chipukizi amejizolea umaarufu wa ghafla haswa tu alipojikuta ameingia kwenye bifu na dancer wa staa wa Marry You na rais wa WCB Diamond Platnumz, Moze Iyobo.

Diamond akihojiwa na Global Online Tv, alieleza kwa undani jinsi anavyomfahamu Harmorapa na maoni yake juu ya rapper huyo ambaye kwa siku za hivi majuzi amekua akitengeneza headlines kila uchao.

Katika mahojiano hayo Diamond alisema hana shida na dogo huyo na kama akitaka collabo na role model wake ambaye yuko chini ya label yake ya WCB Harmonize basi angekuwa wa kwanza kuwa mstari wa mbele kuipa shavu collabo hiyo ili kumuinua staa huyo chipukizi. Nikinukuu maneno yake hapa chini;

“Mi nafikiri kwanza nimpongeze kwanza Harmonize. Kwasababu ukishakua mtu fulani, akatokea mtu fulani labda ni shabiki wako, kwasababu itakuwa Harmorapa ana mapenzi na Harmonize, ina maana kuwa kuna mtu anamtazama kuna mtu kwa namna moja ama nyingine anapitia kwa link yake. Na pia nampongeza Harmorapa kwasababu masikini wa Mungu anatafuta riziki,” alisema Diamond.

Source: bongo5.com

Leave your comment