Tyra Banks Achaguliwa Kuwa Mtangazaji Mpya wa America’s Got Talent
14 March 2017

Tyra Banks amechaguliwa kuwa mtangazaji mpya wa American’s Got Talent.
Mwanamitindo huyo anachukua nafasi ya Nick Cannon kabla ya kupigwa chini na kituo cha runinga cha NBC ambacho kinaonesha show hiyo.
Kupitia mtandao wa Twitter kituo hicho cha runinga kimemthibitisha mremb huyo kuwa ndio mtangazaji mpya kwa kuandika, “America, strike a pose. #AGT has a brand-new host! Welcome to the fam, @tyrabanks!.”
Mrembo huyo pia amewahi kuwa mtangazaji wa America’s Next Top Model kwa misimu 22.
Source: bongo5.com




Leave your comment