TANZANIA: Mwana FA Aelezea Hali ya TID Inavyoendelea Mazoezini

Mwana FA amefunguka hali ya TID Mnyama inavyoendelea tangu alipotangaza kuachana na kutumia madawa ya kulevya na kujikita kwenye kufanya mazoezi zaidi.

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa afya ya muimbaji huyo kwa sasa inaridhisha.

“TID anaendelea vizuri, kwa sababu kwanza TID siyo mtu anayeanza mazoezi sasa hivi. Maisha maisha tu yalikuwa yanampeleka hapa na pale lakini amekuwa anafanya mazoezi kwa muda mrefu kwahiyo inakuwa siyo ngumu kurudisha mwili kwake, mwili unakuwa na tabia ya kukumbuka muscles zina tabia ya kukumbuka,” amesema FA.

“Kwahiyo pengine anapata wakati mgumu wakati anaanza kwa sababu aliacha kwa muda mrefu anakuwa anapata maumivu lakini mara moja tu unaona anaitika. Nafikiri anaendelea vizuri na ukija unakuta yeye ndio amelowa jasho kuliko watu wote gym nzima, yaani anatia moyo,” ameongeza.

Source: bongo5.com

Leave your comment