KENYA: New Video: Muthoni The Drummer Queen – Kenyan Message

Baada ya kimya kirefu, rapper mkali kutoka nchini Kenya Muthoni the Drummer Queen ameachia kichupa chake kipya.

Muthoni ambaye ameipa ngoma hii jina la Kenyan Message, ameandika mashairi yanayolenga wanasiasa kuwakashifu vikali vile wamekuwa wakitelekeza majukumu yao kama viongozi na kuachia wananchi wakiwa wanaumia.

Verse 1 analalama vikali, kwamba tangu apige kura na kumchagua kiongozi wake basi hata simu hashiki tena. Kila akipanga siku kukutana naye mwisho anavunjika moyo kwani kiongozi anasema yuko na shughuli kwengine.

Verse 1.

Tangu ile siku tukuelect,
Haushikagi simu men tuwezi connect,
Nimekua nikisaka na appointment,
Nimekua nikisuffer na disappointment.

Katika mashairi haya ameangazia migomo ya wafanyakazi wa serikali ambayo imekuwa ikishuhudiwa nchini Kenya mara kwa mara mfano ulio hai mgomo wa madaktari na walimu na shida wanazopata wakenya kupitia kwa mikono ya wanasiasa walio wachagua ndio, uchumi ulivyopanda, majanga ya njaa na mengineo maana akaona kuwaandikia wakenya waraka huu kupitia wimbo.

Japo lugha ambayo imetumika kwenye mashairi ya ngoma hii ni Sheng, ambayo ndio inatumika sana hasa Jijini Nairobi, makala haya yamekupa muktadha wa maana halisi ya mashairi ya nyimbo hii.

Source: bongo5.com

Leave your comment