TANZANIA: Barakah The Prince Amtaja Mfalme wa Hip Hop Bongo

Barakah The Prince amemtaja rapper ambaye kwa upande wake ndio mfalme wa muziki wa hip hop Bongo.

Akiongea kwenye kipindi cha Panet Bongo cha EATV Jumatatu hii, muimbaji huyo amemtaja Lord Eyez ambaye yupo chini ya lebo yake ya Bana kwake ndio anamuona kama mfalme wa muziki huo hapa nchini.

“Nimesikia kuna watu wana diss Lord Eyes kusimamiwa kazi zake na mimi. Nachoweza kusema hao ni waoga wanajua Lord ana talent kubwa hivyo wameanza kumuogopa. Mimi namuona Lord Eyes ni mfalme wa hip hop Bongo,” amesema Barakah.

Kwa sasa lebo ya Bana inawasimamia wasanii takribani wanne akiwemo Naj, Lord Eyez na wasanii wengine wawili ambao bado hawana majina makubwa kwenye tasnia ya muziki.

Source: bongo5.com

Leave your comment