TANZANIA: Barakah The Prince Adai Kuwashirikisha Cassper Nyovest na Patoranking

Barakah The Prince ametaja wasanii kutoka nje ya nchi ambao tayari ameshafanya nao kolabo.

Hitmaker huyo wa Nisamehe amemuambia mtangazaji wa kipindi cha Flavour Express cha Maisha FM, Silver Touchez, kuwa tayari ameshafanya kolabo na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini pamoja na Patoranking kutoka Nigeria.

“Kuna my new song inakuja very soon nimefanya na Cassper Nyovest, kuna wimbo tumefanya na Patoranking . Kwahiyo nyimbo zinakuja nyingi but collaboration nyingi zitapatikana kwenye albamu yangu ambayo inatoka mwaka huu,” amesema Barakah.

Muimbaji huyo ameongeza kuwa yeye hafanyi muziki kwa ajili ya kushindana na msanii mwingine bali anafanya kazi nzuri kwa ajili ya mashabiki wake.

Source: bongo5.com

Leave your comment