Sheebah Afanya Remix ya Wimbo ‘Nkwatako’ na Kumshirikisha Solidstar wa Nigeria

Mwanamuziki na dancer wa kike kutoka kundi la zamani la nchini Uganda maarufu kama Obsession lililoundwa na kutamba kwa sana mwaka wa 2006, Sheebah ameamua kuzifuata nyayo za mastaa wengine Afrika Mashariki ikiwemo Eddy Kenzo, Jaguar, Joh Makini, Alikiba, Diamond na wengine wengi na kufanya collabo ya kimataifa na staa wa nchini Nigeria Solidstar.

Sheebah Karungi ambaye baada ya kuvunjika kwa kundi la Obsession aliamua kufanya muziki kivyake, na mwaka 2014 alifanya project yake aliyoipatia jina Ice Cream na kuupa fursa ya kushinda tuzo Hipipo Music Awards za nchini Uganda mwaka wa 2014 na 2015 mtawalia.

Mwaka jana 2016, Shebaah alitamba kwenye ulingo wa sanaa na kibao Nkwatako, ambacho kiliwahi kuwa nominated kwenye Awards za Uganda Entertainment Awards kwa vitengo kadhaa. Kitengo cha kwanza Best Female artist ambacho alishinda, Artist of the year, Best dance/ Live performance,Best dance hall artist na Video of the year ambacho kibao hiki Nkwatako kilimuezesha kuichuna bila ya huruma tuzo hiyo.

Mafanikio haya huenda ndio yamepelekea Sheebah kuvutia baraka za collabo za kimataifa kama hii hapa chini, ambayo pamoja na staa Soldstar wamerudi jikoni na kuuandalia mashabiki wa Africa remix ya Nkwatako.

Uwezo wa Sheeba ni mkubwa kimuziki na huenda mwaka huu akasababisha mambo makuu kimuziki Afrika. Isikilize remix mpya ya Nkwatako hapa chini.

https://www.youtube.com/watch?v=eOXFhGjoRtc&feature=youtu.be

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news