TANZANIA: Wakazi na Nikki Mbishi ni wasanii wa kuwaangalia zaidi mwaka huu

 

 

Fid Q amefafanua kauli yake aliyowahi kuitoa juu ya rapper Wakazi na Nikki Mbishi kuwa ni wasanii wa kuangaliwa zaidi kwa mwaka huu.

Akiongea na Bongo5, Fid amesema, “Nilikuwa najaribu kumulikia mwanga juhudi zao ambazo wamekuwa wakizionyesha kwenye sanaa yao.”
“Kwa mfano mtu kama Wakazi kwa mwaka anaweza akawa na mixtape tatu na ndani yake kunaweza kukawa na ngoma kama nane nane. Wakati huo huo kuna wasanii kwa mwaka wanatoa ngoma moja lakini yupo kwenye mainstream na anafan base kubwa so wanasurvive,” ameongeza.


“Sanaa haihitaji hiyo kitu ila inahitaji variety kwahiyo hawa wamekuwa wakitupa variety, vitu tofauti tofauti kila siku. Kuna wakati Nikki Mbishi alikuwa anatoa ngoma kila wiki.”

Leave your comment