TANZANIA: Dayna Nyange: Kazi Yangu Ijayo Imefanywa Tena na Mr T Touch

Baada ya kufanya kazi takribani tatu mfululizo na mtayarishaji wa muziki nchini Mr T Touch, Dayna Nyange amethibitisha kuwa hata nyimbo yake inayokuja imefanywa na producer huyo.

“Wimbo wangu ujao ninaweza nikasema ndio umefanywa na T Touch kwa sababu ni mtu ambaye ninafanya naye kazi nyingi. Sijafikiria kubadilisha producer kwa sasa, tegemeeni kazi nyingi kutoka kwa Touch lakini kama kutakuwa na mabadiliko yoyote nitawaambia,” amesema Dayna.

Kwa sasa Dayna anafanya vizuri na video ya wimbo wake wa ‘Komela’ ambao ameuachia wiki tatu zilizopita huku ukifanikiwa kutazamwa mara 1.6k kwenye mtandao wa Youtube.

Source: bongo5.com

Leave your comment