TANZANIA:'Muziki' unastahili kuwa wimbo bora wa mwaka 2016 - Darassa

 

Msanii wa rap Bongo, Darassa amefunguka na kusema kuwa kwa mwaka 2016 hakuna wimbo au video iliyofanya vizuri kama ngoma yake hiyo ya 'Muziki' aliyoshirikiana na Ben Pol 


Darassa akizungumza kwenye kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' alidai kuwa wimbo wake huo 'Muziki' unastahili kuwa wimbo bora wa mwaka 2016 na video bora kwa mwaka huo kutokana na kazi hiyo kuchezwa sana karibu kila wakati na kila sehemu.


"Kiukweli kabisa toka ngoma ya muziki imetoka hakuna ngoma nyingine ilikuwa inalia zaidi yake, mimi nitasemaje sasa lazima itakuwa ni ngoma ya 'Muziki' directed by Hanscana, produced by Abba Process na Mr T Touch, acha maneno weka muziki". Alisema Darassa


Mpaka sasa video ya Darassa tangu imetoka tarehe 23 Novemba imefikisha zaidi ya watazamaji milioni 4 kwenye mtandao wa youtube na kuwa video ya kwanza Bongo kwa upande wa wanamuziki wa rap kufikisha watazamaji hao ndani ya muda mfupi.

 

Leave your comment