TANZANIA: 2017 miujiza inaendelea - Darassa

 

 

 

#Muziki ni wimbo uliofana sana mwishoni mwa mwaka 2016, na ni wimbo ambao umeleta taswira mpya ya kimuziki kwa rapa Darassa ambaye amejipatia umaarufu zaidi na kufanya show nyingi huku akishuhudia mambo makubwa zaidi katika muziki wake toka alipoanza kufanya kazi za muziki.

 

Darassa mwenyewe anakiri wazi kuwa mwaka 2016 kwake ulikuwa mwaka wa miujiza kwa jinsi ambavyo ameweza kuja na kubadili upepo wa muziki wa Tanzania na kuingia katika akili za watanzania walio wengi kutokana na kazi yake ya 'Muziki' ambayo imefanya mengi makubwa ndani ya muda mfupi sana.

 

Katika ukurasa wake wa Instagram rapa Darassa aliandika ujumbe ambao unasomeka "2017 miujiza inaendelea" huku baadhi ya mashabiki wake wakitafsiri kuwa rapa huyo ataendelea kufanya vyema na kufanya kazi ambazo huenda zikawashangaza tena kama ilivyokuwa kwa ngoma yake ya 'Muziki'.

 

Leave your comment